Skip to main content
SLU:s publikationsdatabas (SLUpub)

Sammanfattning

Ripoti hii inatoa maelezo mafupi kuhusu uwekezaji mkubwa wa kilimo barani Afrika na nchini Tanzania, pamoja na matokeo ya jumla ya mradi wa utafiti uliofanyika kati ya mwaka 2022–2026 uliotafiti athari za uwekezaji huo nchini Tanzania ambao ulisimama au kufutwa.

Wakati Linda Engström alipokuwa akifanya shahada yake ya uzamivu (PhD) kati ya mwaka 2012–2018, aligundua mwenendo huu na alijaribu kuelewa kwa nini uwekezaji mwingi ulipunguzwa au kufutwa kabisa. Baadhi ya taarifa za msingi katika ripoti hii zinatokana na kazi hiyo. Alitaka kuendelea kuchunguza suala hili, na baada ya kupata PhD yake, yeye pamoja na Ronald Ndesanjo waliomba ufadhili kutoka taasisi ya serikali ya Uswidi. Walifanikiwa kupata ufadhili wa miaka minne kwa ajili ya mradi huu unaohusu uwekezaji mkubwa wa kilimo, ukiweka mkazo hasa kwenye uwekezaji uliosimamishwa au kufutwa, pamoja na upatikanaji na matumizi ya ardhi baada ya wawekezaji kuondoka katika maeneo yao ya uwekezaji.

Lengo la mradi huu lilikuwa kuelewa nini hutokea kwa ardhi inayobaki baada ya wawekezaji kutokuanzisha shughuli zao au kufuta uwekezaji wao. Tulitaka kufahamu ni nani anayepata fursa ya kufikia na kutumia ardhi iliyoachwa na wawekezaji, jinsi wanavyoitumia na sababu za kufanya hivyo. Pia tulitaka kujifunza kutokana na mifano ambapo ardhi ilirudishwa au kugawiwa tena kwa watu waliokuwa wakiitumia au kudai haki juu yake kabla haijatengwa kwa uwekezaji, na/au kwa wahamiaji waliofika baada ya uwekezaji kufutwa.

Mradi ulijumuisha uwekezaji sita katika maeneo matano ya vijijini nchini Tanzania: RAZABA (Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo) katika Wilaya ya Bagamoyo; vijiji vya Basanza na Msebei pamoja na maeneo ya jirani katika Wilaya ya Uvinza; Wilaya ya Kisarawe; na Wilaya za Morogoro Vijijini na Kilosa. Timu ya utafiti ilitumia muda mwingi zaidi katika Wilaya za Bagamoyo na Uvinza. Katika maeneo mengine matatu, tafiti fupi zilifanywa na wanafunzi wa shahada ya uzamili kutoka Tanzania, Norway, Ujerumani na Uswidi.

Muundo wa ripoti: Ripoti inaanza kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusu uwekezaji mkubwa wa kilimo barani Afrika na nchini Tanzania. Kisha inaelezea mradi wa utafiti na baadhi ya matokeo ya jumla yanayohusu uwekezaji wote sita, na baadaye matokeo muhimu kutoka kila uwekezaji. Mwishoni mwa ripoti tunawasilisha timu ya utafiti.

Publicerad i

Utgivare: Chuo Kikuu cha Sayansi za Kilimo, Sweden; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

SLU författare

UKÄ forskningsämne

Jordbruksekonomi och landsbygdsutveckling

Permanent länk till denna sida (URI)

https://res.slu.se/id/publ/146833